" Agape Gospel Band Kuwasha Moto Imba na Yesu Festival 2025!

Agape Gospel Band Kuwasha Moto Imba na Yesu Festival 2025!

 

Tunayo furaha kubwa kuwajulisha rasmi kwamba katika Tamasha la Imba na Yesu Festival Season 2, tutakuwa na waimbaji maarufu wa nyimbo za Injili Agape Gospel Band!

Tamasha hili kubwa litafanyika tarehe 09/05/2025, hapa KKKT Ebenezer Shinyanga, kuanzia saa 2:00 Usiku hadi Saa 12:00 Asubuhi. Agape Gospel Band, maarufu kwa nyimbo zao zenye kugusa roho na kuinua mioyo, wataungana nasi kwa ajili ya kumsifu na kumtukuza Mungu kwa namna ya kipekee.

Kwa mara nyingine, Imba na Yesu Festival inaleta pamoja waimbaji, kwaya mbalimbali, na mashabiki wa muziki wa Injili kutoka sehemu mbalimbali kwa lengo la kusifu, kuabudu, na kuungana katika upendo wa Kristo.

Usikose! Njoo ushiriki nasi katika tukio hili la baraka, lisilo la kawaida, ambapo Agape Gospel Band watafanya huduma ya kusifu kwa nguvu mpya na upako wa kipekee.

👉 Tarehe: 09/05/2025
👉 Mahali: KKKT Usharika wa Ebenezer kanisa kuu Shinyanga
👉 Muda: Kuanzia saa 2:00 Usiku hadi Saa 12:00 Jioni

Wito kwa wote: Njoo, leta familia yako na marafiki, tukamsifu Mungu pamoja kupitia muziki wa Injili unaogusa maisha!

Post a Comment

Previous Post Next Post