Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, Mheshimiwa Liberatus T.K. Sangu, anatarajiwa kuongoza ibada mbalimbali katika kipindi cha Juma Kuu hadi Dominika ya Pasaka mwaka huu wa 2025, katika parokia na makanisa tofauti ya jimbo lake.
Kwa mujibu wa ratiba rasmi iliyotolewa na ofisi ya jimbo, Askofu Sangu ataanza majukumu hayo ya kichungaji leo siku ya Alhamisi Kuu, tarehe 17 Aprili 2025, kwa kuongoza misa takatifu katika Parokia ya Buhangija kuanzia saa 10:00 jioni.
Siku itakayofuata, Ijumaa Kuu tarehe 18 Aprili 2025, atakuwa katika Parokia ya Lubaga ambako ataongoza ibada ya mateso ya Bwana Yesu kuanzia saa 9:00 alasiri.
Katika Jumamosi ya Pasaka, tarehe 19 Aprili 2025, Askofu Sangu atashiriki na kuongoza Mkesha Mtakatifu wa Pasaka katika Kanisa Kuu la Ngokolo, ibada itakayoanza saa 3:00 usiku.
Ratiba hiyo itahitimishwa siku ya Jumapili ya Pasaka, tarehe 20 Aprili 2025, ambapo atasherehekea Dominika ya Ufufuko wa Bwana Yesu Kristo katika Parokia ya Shinyanga Mjini kuanzia saa 2:00 asubuhi.
Waumini wa Jimbo la Shinyanga wanahimizwa kushiriki kwa wingi katika ibada hizo muhimu za Kikatoliki, ambazo ni kiini cha imani ya Kikristo, ili kuadhimisha kwa ibada na tafakari kina cha mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristo.
Post a Comment