Na Daniel Sibu, Misalaba media
Baraza la Wanawake wa Chadema (BAWACHA) Kanda ya Serengeti limeibuka na msimamo thabiti juu ya mustakabali wa uchaguzi nchini, likipinga vikali hatua ya baadhi ya wanachama wa CHADEMA kujitokeza kupinga ajenda kuu ya chama – "No Reform, No Election".
Akizungumza kwa niaba ya wanawake wa Chadema, Rosemary Kirigini, Mwenyekiti wa BAWACHA Kanda ya Serengeti, amesema kwa siku mbili mfululizo wamekuwa kwenye vikao muhimu vya chama wakijadili ajenda mbalimbali, ikiwemo maandalizi ya uchaguzi, lakini pia masuala ya ki chaguzi zisizo huru na haki. Tumekuwa wahanga wa mifumo mibovu ya uchaguzi. Hatuwezi kukubali kurudi kwenye mazingira yale yale. Hii ni vita ya haki, na sisi wanawake tupo mstari wa mbele,” alisema Kirigini.
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, BAWACHA Serengeti imelaani vikali kundi la wanachama wa CHADEMA wanaojiita G55, waliotangaza kutounga mkono ajenda ya No Reform, No Election. Viongozi hao wanawake wamesema kitendo cha wanachama hao kupinga ajenda hiyo ni usaliti kwa juhudi za chama na mapambano ya kisiasa yanayolenga kuleta haki na usawa katika uchaguzi.
“Inasikitisha kuona kiongozi mwenzetu, Mheshimiwa Catherine Luge, ambaye alishuhudia mateso ya kisiasa mwaka 2020, leo anaungana na kundi linalopinga mabadiliko. Kama wanawake, tumesikitishwa sana,” aliongeza.
Wanawake wa Chadema kutoka mikoa mbalimbali ya Kanda ya Serengeti wametangaza msimamo wao kuwa hawatashiriki uchaguzi wa mwaka 2025 iwapo hakutakuwa na mabadiliko ya sheria za uchaguzi na marekebisho ya mfumo mzima wa tume ya uchaguzi.
Msimamo wa BAWACHA:
✅ Tunataka uchaguzi huru na haki.
✅ Tunapinga sheria kandamizi zinazoipa CCM faida isiyo ya
haki.
✅ Tunasimamia ajenda ya "No Reform, No Election"
kwa nguvu zote.
✅ Tunapinga vikali kundi la G55 na msimamo wao wa kuvuruga
umoja wa chama.
Kauli
hii kutoka kwa wanawake wa Chadema Kanda ya Serengeti imeonyesha dhamira ya
dhati ya wanawake katika kuleta mabadiliko ya kweli nchini. Katika wakati ambao
siasa za Tanzania

Post a Comment