" BREAKING: JOHN HECHE AKAMATWA NA POLISI AKIELEKEA MAHAKAMANI

BREAKING: JOHN HECHE AKAMATWA NA POLISI AKIELEKEA MAHAKAMANI

 BREAKING: John Heche Akamatwa na Polisi Akielekea Mahakamani



Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemuweka chini ya ulinzi Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche pamoja na walinzi wake wawili na Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Mara Chacha Heche kwa kile kinachodaiwa kukaidi amri ya kutokwenda Mahakama ya Kisutu kunakotarajiwa kusikilizwa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa chama hicho taifa, Tundu Lissu leo tarehe 24 Aprili 2025.

Hatua hii imejiri baada ya msafara wa Heche kuzuiwa maeneo ya Daraja la Salenda ukiwa njiani kuelekea Mahakama ya Kisutu, na baada ya kile kilichotajwa kuwa mabishano kati yake na Jeshi la polisi, aliamriwa kupanda kwenye gari la polisi ambalo limeonekana kuelekea Kituo cha Polisi cha Oysterbay.

Post a Comment

Previous Post Next Post