" CHADEMA YAELEZA KUTOHUDHURIA KIKAO CHA MAADILI YA UCHAGUZI 2025

CHADEMA YAELEZA KUTOHUDHURIA KIKAO CHA MAADILI YA UCHAGUZI 2025

 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amewataarifu Viongozi wa CHADEMA, Wanachama na Umma wa Watanzania kwamba hatoshiriki, wala hajatuma au kuidhinisha Mwakilishi yeyote kuhudhuria kikao kilichofanyika leo April 12, 2025, Jijini Dodoma, kwa ajili ya kushirikiana na kusaini Maadili ya Uchaguzi wa mwaka 2025.
 
CHADEMA imesema: “Ni muhimu kufahamu kwamba, kwa mujibu wa kanuni za Maadili ya Uchaguzi, Katibu Mkuu ndiye mwenye mamlaka halali ya kusaini maadili hayo kwa niaba ya chama cha siasa.”
 
“Aidha, msimamo huu umetokana na kutokuwepo kwa majibu ya maandishi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu barua rasmi iliyowasilishwa na Katibu Mkuu Desemba 29, 2024, ikieleza mapendekezo na madai ya msingi ya CHADEMA kuhusu mabadiliko ya fumo wa uchaguzi, ikiwa huu unathibitisha kukosekana kwa nia ya dhati ya kufanyika mashauriano ya kweli na ya wazi kuhusu mchakato wa uchaguzi.”
 
“Itakumbukwa kuwa, CHADEMA ilishapitisha maamuzi ya yanayojulikana kama: “No Reforms, No Election” – Bila Mabadiliko, Hakuna Uchaguzi, ambayo yanasimamia hitaji la kufanyika kwa mageuzi ya msingi ya mfumo wa uchaguzi kabla ya kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.”
CHANZO - MILLADAYO

Post a Comment

Previous Post Next Post