Dabi ya Simba na Yanga kupigwa Mei 10 Zanzibar
Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imetangaza rasmi kuwa mechi ya watani wa jadi kati ya Simba na Yanga itachezwa Mei 10, 2025 katika Uwanja wa Amani, Zanzibar.
Kupitia taarifa yake kwa umma, Bodi hiyo imeeleza kuwa uamuzi huo umefikiwa baada ya mashauriano ya kina na pande zote mbili pamoja na wadau wa michezo, huku ratiba ya ligi ikizingatiwa kwa makini. Mechi hiyo inatarajiwa kuanza saa 11:00 jioni.
Post a Comment