" EAST AFRICAN SPIRITS (T) LTD: SAFARI YA MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA VINYWAJI TANZANIA

EAST AFRICAN SPIRITS (T) LTD: SAFARI YA MAFANIKIO KATIKA SEKTA YA VINYWAJI TANZANIA

EAST AFRICAN SPIRITS (T) LTD – FURAHA YA KINYWAJI CHA UBORA WA KIMATAIFA

Malengo ya Uanzishwaji wa Kampuni

Kampuni ya East African Spirits (T) Ltd ilianzishwa mwezi Oktoba 2017, ikiwa na makao yake makuu katika Manispaa ya Shinyanga, Tanzania.
Malengo makuu ya kampuni hii ni kuzalisha vinywaji vya ubora wa hali ya juu vyenye hadhi ya kimataifa ili kukidhi mahitaji ya Watanzania ambayo hayakuwa yametimizwa kikamilifu na bidhaa zilizokuwepo awali.

Awali, kampuni ilianza kwa kulenga kuwahudumia wananchi kupitia bidhaa katika sekta mbili muhimu:

  • Pombe kali (Spirits)
  • Bia

Kwa hatua hii, East African Spirits (T) Ltd imejidhatiti kuwa chaguo sahihi kwa Watanzania wanaotafuta vinywaji bora kwa bei rafiki.


Mafanikio Katika Sekta ya Pombe Kali (Spirits)

Kwa lengo la kufanikisha malengo hayo, mwaka 2017 kampuni ilijenga kiwanda cha kisasa cha kuzalisha pombe kali.
Kupitia kiwanda hiki, kampuni imefanikiwa kutengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu ambazo zimeweza kushindana na bidhaa kubwa za kimataifa.

Bidhaa hizi ni:

  • Hanson's Choice Brandy
  • Diamond Rock Gin

Mrejesho kutoka kwa watumiaji wa bidhaa hizi umeonyesha kuridhishwa kwa kiwango cha juu, wakisifia ladha laini, harufu nzuri, na kutokupata athari ya "hangover" baada ya matumizi.


Mafanikio Katika Sekta ya Bia

Mwaka 2023, East African Spirits (T) Ltd ilizindua kiwanda kipya cha kisasa cha kutengeneza bia kilichopo Shinyanga, Tanzania.
Kupitia kiwanda hiki, kampuni imeweza kuzalisha bia tatu bora ambazo zimepokelewa kwa shangwe kubwa sokoni:

1. Goldberg Malt Lager – 4.4% Alcohol

  • Kauli Mbiu: "Beer of Our Own Class"
  • Bia hii inampongeza mtumiaji kwa kuwa mtu anayejitambua na kuwa katika daraja la kipekee, sambamba na ladha laini ya hali ya juu.

2. Hanson's Lite Lager – 4.0% Alcohol

  • Kauli Mbiu: "The New Lite"
  • Ni bia nyepesi, bora kwa wale wanaotafuta radha ya kipekee bila kuwa na uzito mkubwa wa kilevi.

3. Basembi Extra Lager – 5.8% Alcohol

  • Kauli Mbiu: "Madini, Fahari Yetu"
  • Bia hii inampa mtumiaji chaguo la ladha bora zaidi, yenye vionjo vya kuvutia, isiyoshindanishwa na bia nyingine za daraja la “Lite”.

Mafanikio haya yanaonesha dhamira ya kampuni kumpatia Mtanzania vinywaji vyenye viwango vya kimataifa kwa bei nafuu, bila kumletea madhara kama hangover, huku ikisisitiza unywaji wa kistaarabu kwa watu wa miaka 18 na zaidi.


Kiwezeshi cha Mafanikio

Mafanikio haya makubwa yamewezekana kutokana na:

  • Uwekezaji katika viwanda vya kisasa vilivyowekewa mitambo ya teknolojia ya hali ya juu kama vile:
    • Mitambo ya kusafisha pombe kali kwa kutumia charcoalation ili kupata pombe laini na safi.
    • Mitambo ya kuchuja bia kwa crossflow filtration inayoweka mazingira salama na rafiki.
  • Kutumia wataalamu waliobobea kimataifa, akiwemo Brewmaster anayeheshimika duniani.
  • Kuhakikisha malighafi zote zinakuwa na ubora wa juu na kuidhinishwa na mamlaka za Tanzania na kimataifa, kama vile:
    • Kimea cha shayiri kutoka Ujerumani
    • Shayiri, mchele, na mahindi kutoka Tanzania
    • Maji safi yanayochakatwa kitaalamu kwa uwiano wa madini unaofaa.

Ahadi kwa Watanzania na Dunia

East African Spirits (T) Ltd inawaahidi Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuwa itaendelea kuzalisha vinywaji vyenye ubora wa hali ya juu, hadhi ya kimataifa, na kuzingatia mwelekeo wa mahitaji ya soko.
Kampuni imejizatiti kuwa mstari wa mbele katika ubunifu na utoaji wa bidhaa bora kwa muda wote wa uhai wake.


Hitimisho

East African Spirits (T) Ltd inatoa mwito kwa Watanzania kuendelea kuunga mkono juhudi za ndani kwa kutumia bidhaa zetu.
Kwa pamoja, tutajenga uchumi wetu, kukuza sekta ya viwanda, na kuacha alama kwa vizazi vijavyo.
Tumia vya kwetu – tujenge vyetu kwa ajili ya vizazi vyetu!


Mawasiliano:


🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA


Post a Comment

Previous Post Next Post