Heche Aonana na Tundu Lissu Gerezani, Afunguka Ujumbe Aliyompa
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara John Heche ni mmoja wa Viongozi waandamizi wa Chama hicho waliofika gereza kuu la Ukonga kumuona Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu lissu aliyehamishiwa gerezani hapo akitokea gereza la Keko anaposhikiliwa Mahabusu kwa ajili ya kesi inayomkambili ya uhaini.
Heche amesema ameonana na Lissu akiwa na afya nzuri na kwamba Lissu amewataka CHADEMA waendelee na mapambano bila kurudi nyuma wakati yeye akiendelea kushikiliwa mahabusu.
“Yupo Vizuri ana afya njema ameniambia mapambano yaendelee na Mimi nasema mapambano yaendelee, walimuhamisha kutoka Keko bila kutaarifu Familia na Chama chake na tulifanya jitihada mpaka leo nilipoongea na Viongozi wa juu wa magereza ndio wakatuambia Lissu alipo”
“Timu zilikuwa mbili ya Lissu na Heche baada ya tarehe 24 timu zitakuwa tatu ya Mnyika, Lema na Heche tunavamia kanda ya kati hakuna rangi wataacha kuona hakuna kulala mpaka kieleweke wao wakae na Lissu ndani hakuna kuomboleza”
Post a Comment