" KAFULILA- UCHUMI WA TANZANIA UMEPANDA KWA ONGEZEKO LA ASILIMIA 6

KAFULILA- UCHUMI WA TANZANIA UMEPANDA KWA ONGEZEKO LA ASILIMIA 6

 UCHUMI wa Tanzania umepanda kutoka Dola za Kimarekani bilioni 13 mwaka 2000 hadi kufikia Dola bilioni 85 mwaka 2025 ambapo ni ongezeko la asilimia 6.

Ametoa kauli hiyo Aprili 17,2025 Mkurugenzi Kituo Cha Ubia Kati ya Serikali na Sekta Binafsi David Kafulila kwenye mjadala wa kitaifa ambao ulibeba mada isemayo PPP katika muktadha wa Dira ya Taifa 2050.

Akijibu hoja iliyotolewa katika mdahalo huo Kafulila amesema sarafu peke yake haiwezi kupima kukua kwa uchumi, kwani kuna nchi ambazo sarafu zao ndio zinaongoza, lakini sio zinazoongoza kwenye uchumi.

"Kama sarafu ingekuwa inaongoza uchumi, basi Marekani sarafu yake ingekuwa ya kwanza, lakini sarafu yake ni ya kumi kwa ukubwa duniani". Kafulila amesema

Kafulila ameeleza kuwa katika Dira ya Taifa iliyopita kuna mambo kama nchi imefanikiwa lakini pia amesisitiza baadhi ya mambo kufanyiwa kazi, likiwemo suala la mikopo kwaajili ya shughuli za Maendeleo ikiwemo kilimo ambacho kimeajiri asilimia 65.

Kwa upande wake,Mdau wa mdahalo huo, Elibariki Mmari ameshauri kupitia hoja yake kuwa inapaswa kufanyika utafiti kwa lengo la kusaidia uchumi na sarafu nchini kukua, ikilinganishwa na Dola ya Marekani.

Post a Comment

Previous Post Next Post