" KATIBU MPYA WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA MPANDA JIMOTOLI JILALA MADUKA AANZA KAZI RASMI KWA MAPOKEZI YA KISHUJAA

KATIBU MPYA WA JUMUIYA YA WAZAZI CCM WILAYA YA MPANDA JIMOTOLI JILALA MADUKA AANZA KAZI RASMI KWA MAPOKEZI YA KISHUJAA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Katibu mpya wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Jimotoli Jilala Maduka, ameanza rasmi majukumu yake katika Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, baada ya kuteuliwa hivi karibuni akitokea kwenye Jumuiya hiyo mkoani Shinyanga.

Mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Katavi kwa ajili ya kujitambulisha, Katibu huyo amepokelewa kwa bashasha na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndugu Kinyonto, kwa niaba ya Katibu wa CCM Mkoa huo. Ndugu Kinyonto amemkaribisha rasmi na kumhakikishia ushirikiano wa dhati katika kuhakikisha kazi za chama zinafanyika kwa weledi na tija.

Aidha, Maafisa TEHAMA wa CCM Wilaya ya Mpanda pia wamemkaribisha Katibu huyo kwa furaha na hamasa kubwa, wakieleza kuwa wapo tayari kushirikiana naye kuhakikisha wanachama wa Jumuiya ya Wazazi wanasajiliwa kwa usahihi kupitia mifumo ya kisasa ya chama.

Katibu Jilala Maduka ameonesha utayari wake wa kuwatumikia wazazi na chama kwa ujumla, akisisitiza kuwa ataendelea kudumisha maadili, mshikamano na kuimarisha uhai wa chama katika ngazi ya wilaya kwa ushirikiano wa viongozi wote wa chama na Jumuiya.

Katibu mpya wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Jimotoli Jilala Maduka akipokelewa kwa bashasha na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndugu Kinyonto, kwa niaba ya Katibu wa CCM Mkoa huo leo Aprili 17, 2025. 

Katibu mpya wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Jimotoli Jilala Maduka akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa TEHAMA wa CCM Wilaya ya Mpanda leo Aprili 17, 2025.

Katibu mpya wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda, Jimotoli Jilala Maduka, akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali ikiwemo katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda Masanja ambaye amepongeza kwa uteuzi huo.Jimotoli Jilala Maduka, akisaini kwenye kitabu cha wageni baada ya kuwasili.


Post a Comment

Previous Post Next Post