Umoja wa Waendeshaji Bajaji, Bodaboda na Wajasiriamali jijini Dar es Salaam, umetangaza kutoshiriki maandamano yaliyoitishwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yaliyopangwa kufanyika Aprili 24, 2025, kuelekea Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambako kesi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, inatarajiwa kusikilizwa.
Makamu Mwenyekiti wa Wajasiriamali Wadogo nchini, Steven Lusinde, ametoa tamko hilo leo Ilala Jijini Dar es salaam akisisitiza kuwa wanachama wao wameamua kutumia siku hiyo kufanya kazi na kujitafutia kipato badala ya kushiriki maandamano.
“Hatuko tayari kushiriki maandamano hayo. Siku hizi tunajitambua, hatuna muda wa kupoteza. Tunajikita katika kazi zetu ili kujipatia riziki na kuendeleza maisha yetu,” alisema Lusinde.
Aidha, alieleza kuwa kundi hilo halihusiki na vitendo vya uchochezi na badala yake linahamasisha amani. Pia alikumbusha kauli ya zamani ya kiongozi mmoja wa Chadema aliyewahi kudharau kazi ya bodaboda kwa kuitaja kuwa ni ‘kazi ya laana’, jambo ambalo limewaudhi wahusika wengi.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Maofisa Wasafirishaji nchini, Said Kagomba, alisema kuwa walipokea taarifa kupitia vyombo vya habari kuhusu wito wa Chadema kwa wananchi kujitokeza kwa wingi mahakamani siku hiyo. Hata hivyo, alibainisha kuwa wao hawatahusika na maandamano hayo, huku akiomba mamlaka husika, hasa Jeshi la Polisi, kuchukua hatua za kuhakikisha amani inatawala.
“Leo wanatuhamasisha tushiriki maandamano, lakini hawa hawa waliwahi kudharau kazi zetu—ambazo zimetuwezesha kujenga nyumba, kusomesha watoto wetu na kushiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo,” alisema Kagomba.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Bajaji wenye ulemavu kutoka Kariakoo, Gosbart Kajaraba, alisema kuwa hawana mpango wa kushiriki maandamano hayo kwani wanatambua athari zake kwa amani na shughuli zao za kila siku.
“Tunaamini katika utulivu. Tunahitaji mazingira tulivu ili tuendelee kuzalisha mali na kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali,” alisema Kajaraba.
Nao viongozi wa machinga katika soko la Ilala, wakiongozwa na Bakari Mkupa, walisema
Post a Comment