" Malawi Yatoa Onyo na Kutoa Sababu za Kuzuia Mazao Kutoka Tanzania

Malawi Yatoa Onyo na Kutoa Sababu za Kuzuia Mazao Kutoka Tanzania

 



Waziri wa Biashara na Viwanda wa Malawi Vitumbiko Mumba anasema kuwa nchi ya Malawi imepiga marufuku bidhaa za kilimo kutoka nje ya nchi hiyo, ili kulinda soko la ndani kwa miaka miwili , huku akieleza kuwa Malawi ina haki ya kufanya hivyo.

Akizungumza na gazeti la The Times la nchini Malawi waziri Mumba ameeleza kuwa marufuku hiyo inahusu bidhaa za kilimo kutoka nje ya Malawi ikiwemo Tanzania bidhaa hizo ni pamoja na mchele, matunda, unga wa mahindi, maziwa freshi, mboga mboga na bidhaa nyinginezo, isipokuwa zile ambazo hazilimwi wala kuzalishwa nchini Malawi

Alipoulizwa kuhusu kauli ya waziri wa kilimo wa Tanzania Hussein Bashe kuwa Tanzania itajibu mapigo alijibu kuwa suala hilo linafanyiwa kazi na wao Malawi huwa hawajibu katika mitandao ya kijamii , huku akikiri kuwa Malawi inatakiwa kutumia dirisha la mazungumzo lililofunguliwa na Tanzania na kwani Malawi itapata madhara makubwa ya kiuchumi kama Tanzania itachukua hatua hizo

Waziri huyo ameonya kuwa hatua ambazo Tanzania itazichukua zitakuwa na madhara makubwa ya kiuchumi nchini Malawi, ikiwemo katika uagizaji wa bidhaa za nje zinazotegemea bandari na hivyo ni vyema kutatua suala hilo kwa njia ya mazungumzo

Post a Comment

Previous Post Next Post