Mazishi ya Baba Mtakatifu Fransisko, itafanyika Jumamosi ijayo tarehe 26 Aprili 2025, saa 4:00 asubuhi, mbele ya Kanisa kuu la Mtakatifu Petro huko Vatikani.
Ratiba hiyo ya mazishi imetangazwa na Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia za Kipapa leo tarehe 22 Aprili, 2025, huku ikiripoti kwamba, ibada ya mazishi itaongozwa na Mwadhama Giovanni Kardinali Battista Re, ambaye ni Dekano wa Baraza la Makardinali.
Watu mbalimbali watatoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Papa Fransisko kesho siku ya Jumatano tarehe 23, 2025, ambapo saa 3:00 asubuhi kwa saa za Ulaya, jeneza lenye mwili wa Papa litatolewa kwenye Kikanisa cha nyumba ya Mtakatifu Marta Domus hadi kwenye Basilika ya kipapa ya Mtakatifu Petro, kama inavyoelekezwa katika kanuni ya maziko ya Papa.
Mwili wa Papa Fransisko utapelekwa Basilika baada ya muda wa maombi yatakayoongozwa na Mwadhama Kelvin Kardinali Joseph Farrell, ambaye ni Camerlengo wa Vatikani.
Viongozi kadhaa wa nchi na serikali akiwemo Rais wa Marekani Donald Trump wametangaza ushiriki wao kwenye mazishi ya Papa.
Post a Comment