
Chanzo chetu cha habari kilichowanasa viongozi hao wakiwa kwenye mazungumzo, kimeeleza kuwa wawili hao wamefanya mazungumzo kwa muda wa takribani saa moja, wakijadili na kuzungumza masuala mbalimbali.
Lissu Aprili 10, 2025 alirudishwa mahabusu baada ya kusomewa shitaka la uhaini katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushindwa kujitetea kutokana na kosa hilo kumnyima dhamana na nafasi ya kujitetea, akituhumiwa pia kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X akitarajia kupandishwa tena mahakamani Aprili 24 mwaka huu.
Post a Comment