Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwanaume mwenye umri wa Miaka 35 Athuman Idd , mkazi wa mtaa na kata ya Ndembezi, Manispaa ya Shinyanga, amekutwa amejinyonga katika kata ya Kolandoto, siku moja baada ya kuachiwa kutoka polisi.
Mwenyekiti wa mtaa wa Ndembezi, Mariam Mdoe, amesema
kuwa tukio hilo limetokea siku moja baada ya marehemu kutoka polisi.
Amesema kuwa Jumamosi mwanamke mmoja alifika ofisini
kwake akiomba barua ya dhamana kwa ajili ya mumewe aliyekuwa polisi.
Baada ya kuandika barua hiyo, mwanamke huyo alienda
kumdhamini mumewe. Hata hivyo, siku iliyofuata, yaani Jumapili, alimtafuta kwa
simu na kumjulisha kuwa mumewe amekutwa amejinyonga.
"Ilipofika
Jumamosi, mwanamke mmoja alifika ofisini kwangu akiomba barua ya dhamana kwa
ajili ya mumewe aliyekuwa polisi. Tulimwandikia, akaenda kumdhamini, lakini
siku ya Jumapili alitupigia simu kutupa taarifa kuwa mumewe amefariki dunia
baada ya kukutwa amejinyonga," amesema Mdoe.
Inaelezwa kuwa marehemu Athuman Idd, aliyekuwa na
umri wa miaka 35, alikamatwa na polisi kwa kosa la kuendesha pikipiki akiwa
amelewa na bila kuvaa kofia ngumu.
Jamii imeelezea masikitiko yake kuhusu tukio hilo na
kuwaomba wananchi kuepuka kujichukulia sheria mkononi kwa kujitoa uhai, huku
pia ikihimiza watu kuacha unywaji wa pombe kupita kiasi.
Marehemu ameacha mke na watoto watatu, hata hivyo,
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limesema bado halijapokea taarifa rasmi
kuhusu tukio hilo.
Post a Comment