" Mchungaji Mwamposa Afunguka: Niliwaombea SIMBA Wakashinda.....

Mchungaji Mwamposa Afunguka: Niliwaombea SIMBA Wakashinda.....

 Mchungaji Mwamposa Afunguka: Niliwaombea SIMBA Wakashinda.....

Muhubiri wa Kanisa la Arise and Shine International, Boniface Mwamposa (@Mtume_Boniface_Mwamposa), amesema yeye si Mshabiki wa Timu yoyote bali ni Mchungaji wa Watu wote hivyo hana upande kwenye soka kama ambavyo baadhi ya Watu wamekuwa wakitafsiri baada ya Simba kushinda mechi yao ya kimataifa hivi karibuni.

Akizungumza  katika ibada ya kanisani kwake Mwamposa amesema ni kweli alifanya maombi kwa ajili ya timu ya Simba lakini si kwa sababu anaishabikia bali kwa kuwa mechi hiyo ilikuwa ya kitaifa na ilibeba heshima ya Nchi kimataifa. “Huu si mchezo wa Simba na Yanga ni wa kimataifa Taifa linasimama hawa Watu wa Simba walinipa kazi kubwa ya kuwaombea nikapiga magoti, nikawaombea,” amesema.

Mtume huyo amefafanua kuwa alifanya jukumu lake la kiroho kama kiongozi wa imani na si kama shabiki hivyo Watu wasimtie upande au kumpa sifa za ushindi ambazo si zake. “Wamesema Bulldozer kaombea ndiyo maana Simba wameibuka na ushindi, mimi nilimuomba Mungu tu siyo kwamba nina upande – mimi ni mchungaji wa wote,” amesema.

Kutokana na maombi mengi anayopokea kutoka kwa Watu wanaotaka mafanikio kwenye michezo na maisha kwa ujumla, Mwamposa ametangaza kuwepo kwa mafuta maalum ya upako kwa ajili ya Watu hao. “Sitaki Watu waanze kunipigia simu nimeandaa mafuta ya upako chukueni nendeni mkatumia kwa jina la Yesu na mtapata ushindi,” amesema.

Amesisitiza kuwa hataki kuacha huduma ya kuwaombea Wagonjwa na kuhubiri ili aanze kushughulika na maombi ya soka kila mara hivyo kwa yeyote anayehitaji msaada wa kiroho, milango iko wazi kutumia mafuta hayo kwa imani

Post a Comment

Previous Post Next Post