Na Mapuli Kitina Misalaba
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo
iliyotekelezwa katika shule ya sekondari Bunambiyu, Halmashauri ya Wilaya ya
Kishapu mkoani Shinyanga, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa wiki ya wazazi ngazi
ya mkoa.
Uzinduzi huo unaofanyika leo Aprili 9, 2025 katika
viwanja vya shule hiyo umehudhuriwa na mamia ya wanachama na wananchi,
ukiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Shinyanga, John
Siagi.
Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa miradi hiyo,
Mhe. Mlolwa ameipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia
Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha nyingi za maendeleo kwenye sekta ya
elimu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Shule ya Sekondari
Bunambiyu, Mzee Matata Joel, shule hiyo imepokea zaidi ya shilingi milioni
166.4 kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa ajili ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo.
“Katika
mwaka wa fedha 2021/2022 tumepata fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa na
ofisi; mwaka 2022/2023 tukajenga vyumba viwili vya madarasa; na mwaka 2023/2024
tumekamilisha vyumba viwili vya madarasa pamoja na matundu manne ya vyoo,”
amesema Mzee Matata.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa kati ya shilingi
166,400,000 zilizotolewa na serikali, kiasi cha shilingi 165,892,880.50
kimetumika katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa mafanikio makubwa.
Mara baada ya ukaguzi huo, viongozi wa chama
wakiwemo Mhe. Mlolwa na viongozi wengine wa Jumuiya ya Wazazi wamepanda miti
katika mazingira ya shule hiyo kama ishara ya utunzaji wa mazingira na kuongeza
mvuto wa shule.
Viongozi wengine walioungana na Mwenyekiti Mlolwa
katika uzinduzi huo ni pamoja na Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia
Batimayo; Katibu wa Siasa, Uenezi na Mafunzo Richard Masele; Mwenyekiti wa CCM
Wilaya ya Shinyanga, Mhe. Anord Makombe pamoja na viongozi wengine wa chama na
jumuiya hiyo.
Maadhimisho ya wiki ya wazazi ngazi ya mkoa
yanaendelea kwa kutoa elimu kwa wazazi juu ya masuala ya malezi, maadili,
elimu, afya na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa, akiwasili katika shule ya sekondari Bunambiyu
akiwa na viongozi mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa wa
Shinyanga John Siagi.

Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa akipanda mti katika shule ya sekondari Bunambiyu leo Aprili 9, 2025.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa akipanda mti katika shule ya sekondari Bunambiyu leo Aprili 9, 2025.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mabala Mlolwa akipanda mti katika shule ya sekondari Bunambiyu leo Aprili 9, 2025.
Post a Comment