Kwa heshima na taadhima, Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda imemkabidhi rasmi nyumba ya kuishi Katibu wao mpya, Jimotoli Jilala Maduka, ikiwa ni sehemu ya kumpa mazingira mazuri ya kufanikisha majukumu yake mapya ya kiuongozi.
Makabidhiano hayo yamefanyika baada ya mapokezi
rasmi ya Katibu huyo aliyeteuliwa hivi karibuni, ambapo viongozi wa Jumuiya
hiyo, kwa kushirikiana na Kamati ya Utekelezaji, wameonesha mshikamano na moyo
wa kujali kwa kumpatia makazi rafiki kwa utendaji kazi bora.
Akizungumza mara baada ya kupokea nyumba hiyo,
Katibu Jilala Maduka ameishukuru Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi
pamoja na uongozi mzima wa CCM Wilaya ya Mpanda kwa moyo huo wa kipekee wa
kumkaribisha na kumpa mazingira mazuri ya kazi.
“Nawashukuru sana kwa kunipokea kwa mapenzi makubwa
na kunikabidhi makazi haya. Huu ni uthibitisho kuwa CCM inathamini kazi na utu.
Kwa pamoja tutaendelea kusonga mbele kuwatumikia wanachama wetu kwa uaminifu,
nidhamu na moyo wa kizalendo,” amesema Katibu huyo.
Makabidhiano haya yameongeza hamasa kwa wanajumuiya
wa Mpanda ambao wameonesha furaha yao kwa neno maarufu la hamasa: "Wazazi
Oyeeeeee!"
Kauli mbiu ya "Kazi na Utu – Tunasonga
Mbele” imeendelea kuwa dira ya utendaji katika Jumuiya hiyo, huku viongozi
na wanachama wakiahidi kushirikiana bega kwa bega na Katibu mpya ili kuimarisha
zaidi uhai wa chama.
Post a Comment