" PAPA FRANCIS AFARIKI DUNIA VATCAN ITALIA

PAPA FRANCIS AFARIKI DUNIA VATCAN ITALIA






Papa Francis Enzi ya Uhai

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, alifariki dunia leo Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025, akiwa na umri wa miaka 88 katika makazi yake yaliyopo Casa Santa Marta, Vatican.

Muda mfupi uliopita, Mwadhama Kardinali Farrell alitangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francis kwa maneno haya:

“Ndugu wapendwa, kwa huzuni kubwa sina budi kutangaza kifo cha Baba Mtakatifu Francisko.”

Saa 1:35 asubuhi ya leo (kwa saa za huko), Askofu wa Roma, Francis, alirudi nyumbani kwa Baba. Maisha yake yote aliyaweka wakfu kwa huduma ya Bwana na Kanisa Lake.

“Alitufundisha kuishi maadili ya Injili kwa uaminifu, ujasiri na upendo wa ulimwengu wote, hasa kwa ajili ya maskini zaidi na waliotengwa zaidi.”

Farrell ameongeza: “Kwa shukrani nyingi kwa mfano wake kama mfuasi wa kweli wa Bwana Yesu, tunaipongeza roho ya Papa Francisko kwa upendo wa huruma usio na kikomo wa Mungu Mmoja wa Utatu.”

Kifo cha Papa kimetokea chini ya saa 24 baada ya kuonekana hadharani katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican, kwa ajili ya maadhimisho ya Jumapili ya Pasaka hapo jana.

Alijitokeza akiwa ameketi kwenye kiti cha magurudumu na alipunga mkono kutoka kwenye baraza ya Basilica ya Mtakatifu Petro kwa umati wa watu waliokuwa wakimshangilia, akisema: “Ndugu wapendwa, Pasaka njema.”

Post a Comment

Previous Post Next Post