" PICHA: JOKATE AWASILI KAHAMA KWA AJILI YA TAMASHA LA MWANAMKE CHUMA

PICHA: JOKATE AWASILI KAHAMA KWA AJILI YA TAMASHA LA MWANAMKE CHUMA

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), Jokate Mwegelo, amewasili Wilayani Kahama kushiriki tamasha la Mwanamke Chuma linalofanyika leo Aprili 12, 2025 katika Ukumbi wa Malex Hall, Manispaa ya Kahama.

Jokate anashiriki tamasha hilo kama mgeni rasmi, ambapo wanawake waliotoa mchango mkubwa katika jamii wanatarajiwa kupewa tuzo maalum kama sehemu ya kutambua juhudi zao.

Tamasha hilo ambalo linafanyika kwa msimu wa tatu mfululizo, linaongozwa na kaulimbiu ya kuhamasisha usawa wa kijinsia na kuinua sauti ya mwanamke katika maendeleo ya jamii.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post