" POLISI MKOANI TABORA WAMSHIKILIA AFISA HABARI WA YANGA ALI KAMWE

POLISI MKOANI TABORA WAMSHIKILIA AFISA HABARI WA YANGA ALI KAMWE

 Mange Amuomba Msamaha Mama Dangote, Ataka Waungane Kumuokoa Diamond kwenye mikono ya Zuchu




Polisi Mkoani Tabora imethibitisha kumshikilia Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe.

Kamanda wa Polisi Tabora Richard Abwao amethibitisha kushikiliwa kwa Ali Kamwe na Polisi huku tuhuma zake zikitajwa ni kutoa lugha chafu kwa viongozi wa Serikali.

Kamwe alikuwa na timu yake ya Yanga Tabora kwa mchezo dhidi ya Tabora United ambayo ilimalizika jana kwa Yanga kushinda mabao 3-0.

Kabla ya Mchezo Kamwe anatajwa kuzozana na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Paul Matiko Chacha katika kile kilichotajwa kuwa alikuwa akijibu alichosema RC huyo kuwa Yanga wamekuja na kiherehere mkoani mwake.

Post a Comment

Previous Post Next Post