" PURA KUNADI NA KUWEKA HADHARANI VITALU 26 VYA UTAFUTAJI MAFUTA NA GESI

PURA KUNADI NA KUWEKA HADHARANI VITALU 26 VYA UTAFUTAJI MAFUTA NA GESI

 Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA)  inatarajia kunadi na kuweka hadharani vitalu 26 vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia kwa lengo la kuvutia wawekezaji kuwekeza  katika utafutaji wa mafuta na gesi asilia.

Vitalu hivyo 26 vinavyopatikana katika bahari ya hindi ni 23 na vinavyopatikana na katika eneo la ziwa Tanganyika ni vitalu 3.

Ameyasema hayo leo April 10,2025Jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mkuu PURA, Shigela Malosha katika Mafunzo kwa Wahariri na Waandishi wa habari  yalifanyika kwa lengo la kuwajengea ulewa kuhusiana na  masuala ya utafutaji, uendelezaji na utafutaji wa gesi na Mafuta.

Malosha ameeleza kuwa mwekezaji yeyote mwenye mtaji na Teknolojia ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia atapatiwa nafasi ya kuwekeza ambapo atachangia kukuza uzalishaji na utafiti wa gesi  na mafuta sambamba na kuchangia uzalishaji 

Kwa upande wake,Mwandishi wa habari  Idhaa ya Kiswahili ya Sauti Amerika (VOA), Idd Uwesu amesema  mafunzo hayo yamempatia  nafasi kuongeza uelewa kuanzia Katia hatua ya utafutaji wa gesi na mafuta,uzalishaji,usambazaji na usafirishaji ambapo itamuongezea uweledi katika kazi yake anapotaka kuandika kuhusiana na maudhui yanayohusiana na utafutaji wa mafuta na gesi ataandika kitu sahihi.

Naye,Afisa Uhusiano Mwandamizi kutoka Idara ya Habari Maelezo, Bi. Grace Semfuko amesema  amejifunza vitu vingi  ikiwemo jinsi ambavyo PURA inavyofanya kazi bila kuathiri Mazingira  na shughuli za wananchi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Bw. Shigela Malosha wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa waandishi na wahariri wa habari yaliyofanyika Aprili 10, 2025 Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza uelewa wa wadau hao katika masuala ya utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini.
Mhandisi Ndau Ndau kutoka PURA akiwasilisha mada kuhusu historia ya utafutaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini wakati wakati wa mafunzo kwa waandishi na wahariri wa habari  yaliyofanyika Aprili 10, 2025 Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza uelewa wa wadau hao kuhusu sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PURA, Bw. Shigela Malosha wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa waandishi na wahariri wa habari yaliyofanyika Aprili 10, 2025 Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuongeza uelewa wa wadau hao katika masuala ya utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini
.
Mwanasheria Mwandamizi kutoka PURA, Bw. Abbas Kisuju akiwasilisha mada kuhusu duru ya tano ya kunadi vitalu vya utafutaji wa mafuta na gesi asilia nchini wakati wa mafunzo kwa waandishi na wahariri wa habari yaliyofanyika Aprili 10, 2025 Jijini Dar es Salaam. Mafunzo hayo yaliyoratibiwa na PURA yalilenga kuongeza uelewa wa wadau hao katika masuala ya utafutaji, uendelezaji na uzalishaji wa mafuta na gesi asilia nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PURA Bw. Shigela Malosha (katikati walioketi) katika picha ya pamoja na waandishi wa habari na wahariri walioshiriki mafunzo yaliyoratibiwa na PURA. Pichani pia kuna baadhi ya watumishi na aanagezi kutoka PURA.

Post a Comment

Previous Post Next Post