" RAIS SAMIA ATOA SALAMU ZA POLE KUFUATIA KIFO CHA SHEIKH HASSAN DAHER

RAIS SAMIA ATOA SALAMU ZA POLE KUFUATIA KIFO CHA SHEIKH HASSAN DAHER

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kufuatia kifo cha Sheikh Hassan Daher, aliyekuwa Sheikh wa Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora.

Kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), Rais Samia amesema Sheikh Hassan alikuwa mwalimu wa wengi katika imani, aliyesisitiza upendo, umoja, amani na utulivu wa nchi.

“Natoa salamu za pole kwa familia, Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Ali Mbwana, Waislamu wote, ndugu, jamaa na marafiki,” amesema Rais Samia.

Sheikh Hassan ameelezwa kuwa na mchango mkubwa katika jamii kupitia mafundisho na malezi ya kiroho.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.

Post a Comment

Previous Post Next Post