" RAIS SAMIA MGENI RASMI KWENYE TUZO ZA 'SAMIA KALAMU AWARDS' APRILI 29, 2025 JIJINI DODOMA

RAIS SAMIA MGENI RASMI KWENYE TUZO ZA 'SAMIA KALAMU AWARDS' APRILI 29, 2025 JIJINI DODOMA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Wanahabari maarufu kama Samia Kalamu Awards, itakayofanyika tarehe 29 Aprili 2025, jijini Dodoma.


Tuzo hizi zimeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kwa lengo la kuhamasisha uandishi wa habari za maendeleo, zinazozingatia uchambuzi wa kina, maadili ya kitaaluma, uzalendo, na kuongeza maudhui ya ndani yenye taswira chanya ya nchi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben, alieleza kuwa jumla ya washindi 79 wanatarajiwa kutunukiwa tuzo hizo mwaka huu.

Walengwa wa tuzo ni waandishi wa habari, wachapishaji wa maudhui ya mtandaoni, maafisa habari, watangazaji pamoja na vyombo vya habari kwa ujumla.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post