" RASMI: CHADEMA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI, G55 KUKUTANA KUTOA TAMKO

RASMI: CHADEMA KUTOSHIRIKI UCHAGUZI, G55 KUKUTANA KUTOA TAMKO

  


Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, 
Ndg. Kailima, R. K akifafanua jambo.  

Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Kailima Ramadhan, amesema chama chochote ambacho hakitasaini Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa mwaka 2025 hakitaruhusiwa kushiriki uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka huu pamoja na chaguzi nyingine zote ndogo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa hafla ya kusaini kanuni hizo ambapo ameeleza kuwa hadi sasa vyama 18 kati ya 19 tayari vimesaini, huku Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiwa hakijafanya hivyo.

Kailima amefafanua kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 162(2) cha Sheria ya Uchaguzi pamoja na aya ya 1.2 ya kanuni hizo, ni wajibu kwa vyama vya siasa, serikali na tume kusaini ili kuruhusu ushiriki wao katika mchakato wa uchaguzi.

Akizungumza kuhusu hatua ya CHADEMA kutotia saini, aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, John Mrema, amesema wanatarajia kukutana na kutoa tamko kuhusu namna watakavyoshiriki au kutoshiriki uchaguzi huo.

CHANZO - NIPASHE

CHADEMA JIMBO LA SHINYANGA MJINI

Post a Comment

Previous Post Next Post