Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume ya Taifa ya
Uchaguzi (INEC), Kailima Ramadhan, amesema chama chochote ambacho hakitasaini
Kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa mwaka 2025 hakitaruhusiwa kushiriki uchaguzi
wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka huu pamoja na chaguzi nyingine zote ndogo
kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Kauli hiyo ameitoa wakati wa hafla ya kusaini kanuni
hizo ambapo ameeleza kuwa hadi sasa vyama 18 kati ya 19 tayari vimesaini, huku
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiwa hakijafanya hivyo.
Kailima amefafanua kuwa kwa mujibu wa kifungu cha
162(2) cha Sheria ya Uchaguzi pamoja na aya ya 1.2 ya kanuni hizo, ni wajibu
kwa vyama vya siasa, serikali na tume kusaini ili kuruhusu ushiriki wao katika
mchakato wa uchaguzi.
Akizungumza kuhusu hatua ya CHADEMA kutotia saini,
aliyekuwa Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho, John
Mrema, amesema wanatarajia kukutana na kutoa tamko kuhusu namna
watakavyoshiriki au kutoshiriki uchaguzi huo.
CHANZO - NIPASHE
CHADEMA JIMBO LA SHINYANGA MJINI
Post a Comment