" SERIKALI YATOA SIKU SITA KWA NCHI ZA AFRIKA KUSINI NA MALAWI KUONDOA VIKWAZO VYA KIABIASHARA DHIDI YAKE

SERIKALI YATOA SIKU SITA KWA NCHI ZA AFRIKA KUSINI NA MALAWI KUONDOA VIKWAZO VYA KIABIASHARA DHIDI YAKE




Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wanaotekeleza miradi ya kuwawezesha vijana na wanawake katika sekta ya kilimo Mazao uliofanyika leo Aprili 17,2025 jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna_DODOMA

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania imetoa siku sita Kwa nchi za Afrika Kusini na Malawi kuondoa Vikwazo vya kiabiashara vinavyokwamisha Wakulima na Wafanyabiashara wa Tanzania kuuza bidhaa za Mazao katika nchi hizo.

Wito huo umetolewa Aprili 17,2025 jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe,katika mkutano wa wadau wanaotekeleza miradi ya kuwawezesha vijana na wanawake katika sekta ya kilimo Mazao.

Bashe amesema kuwa hakuna Zabibu zozote wala Apples pamoja na mazao mengine ambayo yanaletwa hapa nchini kutoka nchi hizo za Malawi na Afrika Kusini yataingia hapa nchini bila ya wao kuondoa vizuizi ili mazao ya Tanzania yaingie kuuzwa.

“We are not losers kwenye hili game,kama hawaondoi hakuna zao lolote la kwao litaingia hapa nchini,niwaambie tu wafanyabiashara kwenye hilo hakuna kitakachoendelea,”amesema Bashe.

Aidha amesema serikali kupitia wizara ya kilimo,haijawahi kuzuia mazao ya nchi hizo kuingia hapa nchini sasa iweje wao wazuie mahindi kutoka Tanzania halafu wao wanyamaze kitu ambacho hajiwezekani.

Aidha amefafanua zaidi ya kuwa hakuna mtanzania yoyote ambaye atapoteza maisha kwa ajili ya kukosa kula Apple la kutoka Afrika Kusini au Zabibu za nchi hizo wataendelea kutumia mazao ya hapa nchini.

Bashe amesema kuwa nchi haijawahi kumsumbua jirani yoyote kwenye soko la mazao,mara nyingi wakiwa na njaa wanapiga hodi na kusaidia sasa safari hii hakuna ndizi wala bidhaa yoyote ambayo itaingia hapa nchini.

Hata hivyo Waziri Bashe amewapa pole wafanyabiashara wa hapa nchini kutokana na adha kubwa waliopata wakiwa na mizigo ya mazao ya mahindi kupeleka katika nchi hizo.

Amesema wasiwe na wasiwasi wowote kila kitu kitaakaa sawa na kuongeza kuwa safari hii hakuna bidhaa yoyote ya kilimo ambayo itapokelewa kama nchi hizo hazitafungua mipaka hiyo.

Bashe amesisitiza kuwa wafanyabiashara wasibebe kitu chochote kutoka katika nchi hizo

Post a Comment

Previous Post Next Post