Na Belnardo Costantine, Misalaba Media.
Jeshi la Somalia kwa ushirikiano na Marekani wamefanya mashambulizi ya anga na kuwaua wanamgambo kadha wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab waliokuwa wakiushambulia mji muhimu na kambi ya kijeshi nchini Somalia.
Mashambulizi hayo yalifanywa katika mji wa Adan Yabaal, takriban kilomita 220 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu ambao wapiganaji wa Al-Shabaab walipovamia mji huo muhimu wenye kambi ya makamanda wa kijeshi wa Somalia.
Sambamba na hilo Mashambulizi mengine yaliwaua wapiganaji 35 katika mji wa kusini magharibi wa Baidoi..
Post a Comment