" SIKU YA MALIKALE;WATANZANIA WAKUMBUSHWA KUZITEMBELEA MALIKALE ZILIZOPO NCHINI

SIKU YA MALIKALE;WATANZANIA WAKUMBUSHWA KUZITEMBELEA MALIKALE ZILIZOPO NCHINI













Mhifadhi Mkuu Mambo ya Kale na Mkuu wa Kanda ya Magharibi Makumbusho na Malikale anayesimamia uhifadhi na uendelezaji maeneo ya kusini mwa Tanzania Lindi na Mtwara Revocatus Bugumba akizungumzia siku ya Kimataifa ya Malikale ambayo hufanyika tar 18 April ya kila mwaka.



Mhifadhi Mkuu Mambo ya Kale na Mkuu wa Kanda ya Magharibi Makumbusho na Malikale anayesimamia uhifadhi na uendelezaji maeneo ya kusini mwa Tanzania Lindi na Mtwara Revocatus Bugumba akionyesha jengo la Makumbusho ya awali ambalo sasa linabaki kama malikale.

…………………

NA MUSSA KHALID

Watanzania wametakiwa kushiriki kutembelea maeneo ya Malikale zilizopo nchini ikiwemo kuzuia uharibifu wake ili waweze kujifunza historia ya nchi yao.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mhifadhi Mkuu Mambo ya Kale na Mkuu wa Kanda ya Magharibi Makumbusho na Malikale anayesimamia uhifadhi na uendelezaji maeneo ya kusini mwa Tanzania Lindi na Mtwara Revocatu Bugumba wakati akifanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi katika kuadhimisha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Malikale ambayo hufanyika tar 18 April ya kila mwaka.

Bugumba amesema kuwa Malikale zinajumuisha maeneo na kumbukumbu za kihistoria ambayo yanahifadhiwa ikiwemo majengo ,bustani,maeneo ya kumbukumbu za kivita.

Akitolea mfano wa mji wa Dar es salaam kumesheheni maeneo ya majengo ya kale kama makanisa,mahekalu ya wahindi,majengo ya kiserikali ,maeneo ya mnazi mmoja,majengo kuanzia Ikulu na hata bustani za kale.

‘Kiujumla maeneo mengi ya Malikale huwa yanaathiriwa kwa changamoto za kiasili ambazo ni kama mabadiliko ya Tabia ya nchi,mvua kali ukame na kutokea kwa matukio makubwa yakiwemo vita” amesema Bugumba

Amesema msingi wa dhima ya Malikale imesisitiza kufanya ukusanyaji wa kumbukumbu ikiwemo kufanya tathmini ya maeneo ya malikale na kuyaweka kwenye orodha jambo ambalo litazuia uharibu.

Bungua amesema mpango mwingine ni kusisitiza jamii ishirikishwe kwa namna mbalimbali lakini pia usimamizi kuhakikisha inatumiwa mbinu za asili za uhifadhi za Malikale ili kuepukana na mtindo wa kuondoa thamani ya maeneo hayo na kuweka vitu vya kisasa.

Pia ametumia fursa hiyo kuisistiza jamii kutoa taarifa kuhusu Malikale zilizopo kwenye maeneo yao ambazo zinataka kuharibiwa ili ziweze kuhifadhiwa kwa muda mrefu.

Katika hatua nyingine ,Bugumba ametoa rai kwa Mamlaka za serikali za mitaa kuendeleza maeneo ya Malikale zilizopo kwenye miji yao ili kutopoteza uhalisia na historia ya maeneo hayo.

Mwaka huu 2025 maadhimisho hayo yanakwenda na kauli mbiu ya kuangazia madhara ya majanga na migogoro katika maeneo ya Malikale lakini pia kutafakari miaka sitini ya utekelezaji wa baraza la kimataifa la Malikale katika kutatua migogoro ya malikale na kushughulikia majanga yanayoathiri malikale hizo.


Post a Comment

Previous Post Next Post