Licha ya ushindi huo muhimu, kikosi cha Simba kilikosa nafasi kadhaa za wazi ambazo zingewawezesha kupata ushindi mkubwa zaidi. Mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa Aprili 27, 2025, kwenye Dimba la Moses Mabhida, mjini Durban, Afrika Kusini.
Mshindi kati ya Simba na Stellenbosch atakutana na mshindi wa mechi kati ya RS Berkane ya Morocco na CS Constantine ya Algeria katika fainali ya michuano hiyo ya kimataifa.
Kupitia mitandao ya kijamii, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pongezi kwa wachezaji na benchi la ufundi la Simba SC, akisema:
"Hongera sana kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF Confederation Cup). Mmeleta furaha kwa mashabiki wenu na Watanzania wote na kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu. Motisha kutoka kwangu mtaipokea kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Ninawatakia kila la kheri."
— RAIS SAMIA
Simba sasa wanahitaji sare yoyote au ushindi katika mchezo wa marudiano ili kujihakikishia nafasi ya kucheza fainali ya kihistoria ya CAF Confederation Cup.
Post a Comment