" SIMBA WAKAE KIASKARI, STELLENBOSCH FC WAANZA KUTUPA VIJEMBE

SIMBA WAKAE KIASKARI, STELLENBOSCH FC WAANZA KUTUPA VIJEMBE

 Simba SC Yaanza Kupokea Vijembe Kutoka Stellenbosch, Wakae Kiaskari


Kuelekea mchezo wa marudiano wa CAFCC dhidi ya Simba SC, klabu ya Stellenbosch FC kutoka Afrika Kusini imeonyesha uhakika wa kushunda mchezo na hamasa kubwa mashabiki na wachezaji. Kupitia ujumbe katka mitandao ya kijamii, klabu hiyo imejitambulisha kwa jina la "Lion" (maana yake Simba), ikiashiria kuwa watakuwa wakikabiliana na "Simba" wengine kutoka Tanzania.

"Kupitia ukurasa wa habari wa J Sports Updates, walilipoti maneno ambayo yaliandikwa na kurasa wa Facebook wStellenbokusem, ambapo Klabu hiyo kutoka Durban Afrika Kusini imetakwa kwa kusema kuwa, "Mechi inaenda kuwa kati ya Simba na Simba. Simba wengine wanakuja nyumbani ambapo watakuta simba wengine wanawasubiri, wacha tusubiri siku ya Jumapili alafu tutaona".



Kauli hii inakuja baada ya ushindi mdogo wa Simba SC wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa nyumbani, visiwani Zanzibar. Matokeo hayo yanaifanya mechi ya marudiano kuwa muhimu sana na ngumu kwa timu zote mbili.

Kikosi cha Simba SC kinatarajia kusafiri kesho Jumatano, Aprili 23, kwa ndege ya Air Tanzania kuelekea Afrika Kusini. Msafara huo utaondoka majira ya saa 4:00 asubuhi, ni siku nne kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Aprili 27 2025. Simba wana matumaini ya kulinda faida yao ili kufuzu. Hata hivyo, Stellenbosch wanaonekana kuwa na kiu ya kulipiza kisasi mbele ya mashabiki wao.

Kupitia ujumbe wao, Stellenbosch FC wameanzisha vita ya maneno, wakijitambulisha kuwa na wao ni Simba "Lion" mwingine ambaye anamsubiri "Simba" kutoka Tanzania. Mashabiki wanangojea kuona ni "Simba" gani atatoka na ushindi Jumapili na kufuzu kuingia Fainali.


Kwa mtazamo wako, unaamini ni Simba gani anaenda kushinda kati ya Simba wa Tanzania na Simba wa Afrika Kusini?. Tuandikie maoni yako hapo chini asante.

Post a Comment

Previous Post Next Post