Dar es salaam,
24 April 2025.
TAARIFA KWA UMMA.
Hekima na Umoja;
Kwa huzuni kubwa, Mwenyekiti wa Jumuiya ya SMAUJATA Taifa Shujaa Sospeter Bulugu, na Menejimenti ya SMAUJATA, imepokea taarifa za mauaji ya mwanafunzi wa chuo cha Ustawi wa Jamii kampasi ya Dar es salaam Elizabeth Emmanuel Maguha aliyekuwa akisoma shahada ya kwanza ya menejimenti ya rasilimali watu. Marehemu Elizabeth alishambuliwa kwa kuchomwa kisu mara tatu na mtu anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake wa zamani maeneo ya Yombo Dovya,Temeke alipokuwa anaishi.
Jumuiya ya SMAUJATA kupitia Idara yake ya Wanafunzi, Vyuo na Vyuo Vikuu inalaani vikali vitendo vya kinyama na kikatili vya namna hii, ambavyo ni kinyume na misingi ya utu,haki za binadamu,sheria za nchi na maadili ya kitanzaia.
Mashujaa wa SMAUJATA, tunawapa pole familia,ndugu,Uongozi na Wanafunzi wa Chuo cha Ustawi wa Jamii kufuatia tukio hili baya na la kusikitisha.
SMAUJATA kupitia Kampeni yake ya Kataa Ukatili Wewe ni Shujaa tunawasihi kutoa taarifa mapema pindi muonapo viashiria vya ukatili wa aina yoyote katika madawati ya jinsia, Vituo vya Polisi au kupiga namba 116 ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Bwana alitoa, na Bwana ametwaa — jina la Bwana lihimidiwe.
Post a Comment