
Tamasha kubwa la Mwanamke Chuma 2025 linatarajiwa
kufanyika tarehe 12 Aprili 2025 katika ukumbi wa Malex Hall mjini Kahama,
likiwa na lengo la kuwaunganisha wanawake kutoka nyanja mbalimbali kwa ajili ya
kujadili masuala ya haki za wanawake, ujasiriamali, afya, elimu na usawa wa
kijinsia.
Katika tamasha hilo linaloandaliwa na Gold FM, mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa CCM (UVCCM), Jokate
Mwegelo, huku wageni wengine wa serikali na taasisi binafsi pia wakitarajiwa
kuhudhuria.
Tamasha hilo limebeba dhamira ya kutoa heshima na
kutambua mchango wa wanawake waliovuka vikwazo mbalimbali katika jamii.
Katika tamasha hilo, zitatolewa tuzo mbalimbali
kutambua mchango wa wanawake katika nafasi tofauti ikiwemo uongozi,
ujasiriamali, elimu, afya, na harakati za kijamii, ikiwa ni njia ya kuthamini
na kuhamasisha juhudi zao katika kuleta maendeleo ya jamii.
MISALABA MEDIA tunatarajia kurusha mubashara (live)
tamasha hili kupitia channel ya YouTube.
Post a Comment