IMBA NA YESU FESTIVAL SEASON 2 - 2025
Usiku wa Kusifu na Kuabudu wa Kukumbukwa Unakaribia!
Baada ya mafanikio makubwa ya tamasha la mwaka jana, tamasha kubwa la kusifu na kuabudu linarejea tena kwa kishindo kikubwa! Mwaka uliopita, nyoyo ziliguswa, na sifa zilipaa hadi mbinguni. Ile siku ilijaa utukufu wa Mungu, ulishuhudiwa na mamia ya watu waliokusanyika kwa moyo mmoja na mwaka huu, hali ni tofauti zaidi: kamati imejipanga vizuri kuliko hapo awali!
Kama ulidhani umeyaona yote, jipange upya, kwa sababu mwaka huu utashuhudia kiwango kingine cha uwepo wa Mungu kupitia sifa na ibada.
Kwaya mbalimbali kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Shinyanga tayari zimealikwa na zinatarajiwa kuhudumu siku hiyo kwa moto wa kipekee wa kiroho. Ni wakati wa watu wa Mungu kuungana tena kwa sauti moja ya sifa na ibada, kwa usiku mzima wa kuinua jina la Bwana.
Waimbaji mashuhuri wa muziki wa Injili kutoka maeneo mbalimbali nchini wanatarajiwa pia kualikwa nyota watakaogusa mioyo na kuinua mioyo ya watu kwa uimbaji wa kiungu na wenye upako.
Tamasha litaanza saa 2:00 usiku hadi saa 12:00 asubuhi Mahali ni KKKT Usharika wa Ebenezer Kanisa kuu Shinyanga.
Tamasha hili si la kukosa waambie familia, marafiki na kanisa lako lote. Mungu anaenda kufanya jambo jipya!
“BWANA ameketi juu ya sifa za watu wake.” – Zaburi 22:3
Post a Comment