" TAMWA NA TCRA WATANGAZA MABADILIKO YA SAMIA KALAMU AWARDS 2025

TAMWA NA TCRA WATANGAZA MABADILIKO YA SAMIA KALAMU AWARDS 2025



Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kimetangaza mabadiliko ya tarehe na mahali pa kufanyika kwa hafla ya utoaji wa Tuzo za Uandishi wa Habari za Maendeleo – Samia Kalamu Awards 2025.

Awali, hafla hiyo ilikuwa imepangwa kufanyika Aprili 29, 2025 katika Ukumbi wa Mabele, Mabeyo Complex jijini Dodoma. Hata hivyo, kutokana na sababu za kiutendaji zisizoweza kuepukika, hafla hiyo sasa itafanyika Mei 5, 2025 jijini Dar es Salaam, katika ukumbi ambao utatangazwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA, Dkt. Rose Reuben, na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dkt. Jabiri Bakari, wageni wote waliokuwa wamealikwa awali watapokea mialiko mipya itakayoweka bayana eneo na ratiba kamili ya tukio hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya kipekee ambayo inalenga kutambua na kuenzi mchango wa wanahabari katika maendeleo ya taifa.

TAMWA na TCRA wamewaomba radhi washiriki wote kwa usumbufu uliotokana na mabadiliko hayo na kuwasihi waendelee kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya hafla hiyo. 

Post a Comment

Previous Post Next Post