" TANZANIA NA SWEDEN KUSHIRIKIANA KUIMARISHA MIFUMO YA UBUNIFU

TANZANIA NA SWEDEN KUSHIRIKIANA KUIMARISHA MIFUMO YA UBUNIFU

 NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) mkataba wa miaka mitano na Serikali ya Sweden kwa lengo la kuwezesha tafiti za mabadiliko ya tabia nchi, kuimarisha mifumo ya ubunifu na mawasiliano ya sayansi kwa vyuo vikuu na kuimarisha mawasiliano ya kisayansi.

Thamani ya makubaliano hayo ya mashirikiano ni Shilingi bilioni 10 ambapo bilioni 8.2 zitaletwa nchini na zitakazo salia zitabakia kwa washirika hao.

Akizungumza leo Aprili 3,2025 wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu amesema makubaliano hayo yanaiunganisha serikali ya Tanzania kupitia COSTECH pamoja na serikali za Swedeni kupitia SIDA na serikali ya Norway kupitia NORAD.

Amesema kupitia Sweden iliwasaidia kupata fedha kutoka Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD) waliofadhili tafiti 40 za mabadiliko ya tabia nchi.

‘’Kwenye kongamano sayansi, teknolojia na ubunifu (STiCE) mwaka 2024, tulitoa hundi ya Sh bilioni 6.3 kwa ajili ya watafiti 19 wa mabadiliko ya tabia nchi na wengine tuliwaahidi tutawapatia, kupitia fedha hizi, watafiti 21 waliosalia watapatiwa fedha kwa ajili ya kukamilisha tafiti zao,’’ amesema.

Amesema hiyo ni mara ya nne kwa Costech na Sweden kusaini makubaliano hayo na kwamba kwa kipindi chote cha ushirikiano, ilidhamini miradi 53 ya utafiti na ubunifu katika viwanda, bioteknolojia, uvuvi, kilimo, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, maji, ufugaji na afya.

‘’Wafanyakazi 73 wa Costech walipata mafunzo ya usimamizi wa utafiti, fedha za utafiti, mawasiliano ya utafiti, ubunifu kwa maendeleo ya uchumi, mfumo wa usimamizi ubora, usimamizi wa fehda na haki miliki,’’ ameeleza Dk Nungu.

Pamoja na hayo,Nungu ameishukuru serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka mazingira wezeshi kwani taasisi nyingi zinatamani kufanya nao makubaliano.

Kwa upande wake, Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Charlotta Macias amesema anajivunia kuwaa ufadhili wao umeboresha michakato ya COSTECH ya kutoa ruzuku za utafiti, na kusababisha kuundwa kwa mwongozo mpya wa ruzuku.

Amesema Norway imeungana nao katika utafiti wa hali ya hewa, huku Sweden ikichangia USD milioni 2.5 zaidi. Juhudi hizi zinaimarisha ujuzi wa COSTECH katika kusimamia wito wa utafiti na ushirikiano, na utafiti ambao utaleta suluhisho linalohitajika kwa ajili ya mabadiliko ya hali ya hewa nchini.

Utafiti huo utajumuisha vyuo vikuu nchini vikiwemo MUHAS, UDSM,COSTECH. KTH-Chuo cha Teknolojia cha Kifalme ambapo kitaunga mkono kuendeleza mfumo wa kitaifa wa ubunifu unaohusisha Taasisi na jamii, hata hivyo pia Ofisi ya Haki Miliki ya Sweden (PRV) itafundisha mashirika kutumia taarifa kwa ufanisi,

Post a Comment

Previous Post Next Post