Na Mapuli Kitina Misalaba
Taasisi ya TK Movement Wilaya ya Shinyanga Mjini
imezindua rasmi Wiki ya Vijana na Wanawake kwa kukabidhi msaada wa mashine ya
kunakili (photocopy) kwa Shule ya Msingi Mwamagunguli A, iliyopo Kata ya
Kolandoto, Manispaa ya Shinyanga.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mratibu wa TK
Movement Wilaya ya Shinyanga Mjini, Moses Mshagatila, amesema shughuli hiyo ni
sehemu ya ratiba ya wiki hiyo, ambayo inalenga kuunga mkono juhudi za serikali
katika kuboresha sekta ya elimu.
"Tunatarajia kufanya kongamano la
vijana na wanawake, ambalo limeratibiwa na TK Movement Wilaya ya Shinyanga
Mjini. Leo tarehe 2 tumefungua wiki hii kwa kukabidhi msaada huu wa mashine ya
kunakili. Kesho, Alhamisi, tutakuwa na zoezi la kuchangia damu salama, Ijumaa
tutatembelea vituo vya kulelea watoto yatima na watoto wenye uhitaji, na kilele
cha Wiki ya Vijana na Wanawake kitakuwa Jumamosi tarehe 5 Aprili 2025, kwenye
ukumbi wa Chuo cha Walimu SHYCOM. Tunatarajia mgeni rasmi awe Naibu Waziri wa
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Paschal Patrobas
Katambi," amesema Mshagatila.
Baadhi ya walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi
Mwamagunguli A wameishukuru TK Movement kwa msaada huo, wakieleza kuwa
utarahisisha upatikanaji wa nyaraka muhimu za kitaaluma na kuboresha mazingira
ya kujifunzia.
Mashine hiyo ina thamani ya zaidi ya shilingi
milioni mbili.
Mratibu wa TK Movement Wilaya ya Shinyanga Mjini,
Moses Mshagatila akizunguma.
Post a Comment