" TUWAJENGEE UWEZO WANA-CCM KUJIBU HOJA ZA WAPINZANI -SAGINI

TUWAJENGEE UWEZO WANA-CCM KUJIBU HOJA ZA WAPINZANI -SAGINI

Mbunge wa Jimbo la Butiama na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Jumanne Sagini ameeendelea na Ziara ya kusikiliza na Kutatua kero za wananchi Kata ya Buswahili ambapo amewataka wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi kujibu hoja za wapinzani kwa kuwaonesha maendeleo yaliyofanywa na Rais, Mbunge na Diwani.

Mbunge Sagini amesema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu kuna watu watapita na kupinga kuwa viongozi waliopo madarakani hawajafanya maendeleo ili wapate nafasi ya kujinadi wao hata uchaguzi wa ndani ya Chama Cha Mapinduzi pia, hivyo ndio muda wa kuwaaambia kilichofanyika kuanzia ngazi ya shina mpaka Taifa.

"Hata uchaguzi wa ndani ya Chama Cha Mapinduzi utashangaa kuona baadhi ya wananchama wanaotaka nafasi wanaanza kupinga na kubeza kazi zilizofanyika kipindi hiki kwa lengo la kupata nafasi muwaambie kuwa miradi ya mabilioni imeingia Kata ya Buswahili na utekelezaji umeonekana na vingine vimetekelezwa kwa pesa binafsi za mbunge muwaoneshe Barabara, Kituo cha Afya, Shule taasisi binafsi nk"
 
Mbunge Sagini ametolea mfano kuwa katika kipindi chake Kijiji cha Buswahili kwenye Shule ya Sekondari BUKO zimejengwa maabara tatu ambazo za Fizikia, Kemia na Bailojia pia akiwa kwenye mchakato wa ukarabati wa Shule ya Msingi Buswahili ambayo inamechakaa na kufufua mradi wa kilimo kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi lakini baadhi watasema hatujapiga hatua.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buswahili Mhe. Kisangure Chacha amempongeza Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Jumanne Sagini kwa kusukuma maendeleo katika Kata yake  kama ujenzi wa Kituo cha Afya Kijiji cha Wegero, Ujenzi wa Madarasa na Usajili Shule ya Nyandewa Kijiji cha Buswahili, ukamilishaji wa Nyumba za walimu na kupeleka walimu wa kike Kongoto.

Aidha, ameongeza kuwa Mbunge Sagini amechochea na mpaka umepatikana mradi wa maji wa shilingi milioni 800 ambao utahudumia vijiji vyote (Buswahili, Kongoto, Wegero na Baranga) ambapo mkandarasi ataanza kazi muda si mrefu, amesema alimuomba Mbunge Sagini na akasaidia ujenzi wa madaraja makubwa matatu kwenye Kata yake ambayo yalikuwa kero kwa muda mrefu na ambapo amewashika mkono katika ujenzi na ukarabati ofisi CCM matawi yote


 



Post a Comment

Previous Post Next Post