Na Mapuli Kitina Misalaba
Masuala ya ulinzi na usalama wa watoto wenye umri wa kuanzia miaka 0 hadi 8 yamepewa kipaumbele katika mjadala maalum uliofanyika leo katika kituo cha redio Jambo FM, ukihusisha wataalamu wa masuala ya ustawi wa jamii na ulinzi wa mtoto.
Katika mjadala huo, Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga, Lydia Kwesigabo, amesema watoto wengi wa umri mdogo wanakumbwa na vitendo vya ukatili kutokana na wazazi kukosa muda wa kushiriki kikamilifu katika malezi na makuzi yao.
Kwa upande wake, Inspekta wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Jane Mwanzebe, amebainisha kuwa baadhi ya watoto wanakumbwa na vitendo vya ukatili wakiwa ndani ya familia au kwa watu wanaowaamini.
Aidha, Anascolastica Ndagiwe kutoka Asasi ya Wanawake Laki Moja amesisitiza umuhimu wa elimu ya malezi kwa wazazi na walezi, huku akieleza kuwa familia nyingi zinahitaji msaada wa kitaalamu kujua namna bora ya kuwalea watoto katika mazingira salama.
Katibu wa SMAUJATA Kanda ya Ziwa, Daniel Kapaya, ametoa wito kwa jamii kushirikiana kwa karibu katika kutokomeza ukatili dhidi ya watoto kwa kutoa taarifa za matukio mapema na kushiriki katika ulinzi wa watoto katika maeneo yao.
Mjadala huo umeonesha kuwa bado kuna changamoto kubwa katika malezi ya watoto wadogo, hasa ukosefu wa upendo, ulinzi, na msaada wa kisaikolojia kutoka kwa wazazi na walezi, hali inayohitaji jitihada za pamoja kuirekebisha.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment