" Uwepo wa G55 ni Kukua Kwa Demokrasia 'Lissu Kaeni Mjadiliane' Olengurumwa

Uwepo wa G55 ni Kukua Kwa Demokrasia 'Lissu Kaeni Mjadiliane' Olengurumwa

 Uwepo wa G55 ni Kukua Kwa Demokrasia 'Lissu Kaeni Mjadiliane' Olengurumwa



Akishauri na kukitaka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kuketi na kuzungumza na kundi la G55 (Watia nia ya ubunge 2020 na 2025 wanaopingana na vuguvugu la 'No reforms, No election" Wakili na mtetezi wa haki za binadamu Onesmo.Olengurumwa, ameeleza kuwa uwepo wa kundi hilo ndani ya Chadema ni dalili ya kukuwa kwa demokrasia na Uongozi bora ni pamoja na kuwasikiliza wenye maoni tofauti.

Kupitia ukurasa wake wa X, Olengurumwa ameandika;

"Nimefuatilia Mjadala ndani ya CHADEMA, nina andika kwa ufupi hapa lakini bado nitamtafuta Mhe Lisu @TunduALissu

Miaka zaidi ya 30 iliyopita Wabunge Wapatao 55 wakiongozwa na Mzee Njelu Kasaka waliunda kundi la Wabunge G55 kwa lengo la kutaka kuonyesha kuna mambo hawakubaliani nayo ndani y’a CCM na katika Taifa kwa ujumla likiwemo Muundo wa Muungano. Wakapeleka Hoja Binafsi Bungeni.

Baadaye Serikali iliunda kamati iliyoongozwa na Waziri wa Sheria Mzee Sita pamoja na wajumbe wengine wakiwa Edward Lowasa, Anne Makinda na Seif Khatib. Tume hii iliwasikiliza lakini hawakufkia mwafaka hadi Nyerere akawaita na kuwasilikiza wakiwa na Waziri Mkuu Malecela.

Ushauri wangu

Kama enzi cha chama kimoja walitoka watu wakatoa maoni yao kwa njia ya kutaka kuwa na hoja binafsi, nadhani kuwepo kwa watu wenye mawazo tofuauti ndani ya chama au serikali leo hii ichukuliwe kama ni kukua kwa democracy na uhuru wa maoni.

Mimi na washauri sana viongozi wa Chadema wa juu tafuteni nafasi y’a kuwasikiliza hawa wanachama wenu. Uongozi bora ni pamoja na kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za ndani kwa kuwapa nafasi wenye maoni tofauti na kusikiliza hoja zao.

Wengi tunapenda sana kuona utulivu katika vyama vya siasa kwa kuwa ndio njia pekee ambayo watanzania wanaweza shiriki uongozi wa nchi.

Rafiki zangu Lisu , Heche , Lema na Mnyika tafuteni namna Mkae na G55 yenu. Tupo tayari kusaidia majadiliano haya kati ya Uongozi wa chama na G55. Tuendeleze utamaduni wa mazungumzo pale tunapotofautiana kimitazamo.

Post a Comment

Previous Post Next Post