Na Respice Swetu, Kasulu
Wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita katika shule ya sekondari ya Muyovosi iliyopo halmashauri ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, wameahidi kufanya vizuri katika mitihani yao itakayoanza Mei 5 mwaka huu.
Hayo yamesemwa katika risala ya wahitimu wa kidato cha sita wa shule ya sekondari ya Muyovosi, kwa mgeni rasmi John Kawau aliye mwakilisha meneja wa benki ya NMB tawi la Kasulu.
Wamesema kuwa katika kipindi cha miaka miwili waliyokaa shuleni hapo, wamepata msaada mkubwa wa kimalezi, kimaadili na kimasomo na kuwafanya kuwa na uhakika wa kufaulu kwa kishido kwenye mitihani hiyo.
“Walimu wetu wametuandaa vema kufanya mitihani, na sisi tunaahidi kuwa tutapata ufaulu wa kishindo kwa kuwa tumejiandaa vizuri”, ilisema sehemu ya risala yao.
Akizungumzia mafanikio ya kitaaluma ya shule hiyo, mkuu wa shule ya sekondari ya Muyovosi Nhiga Mwandu amesema, ufaulu wa shule ya sekondari ya Muyovosi iliyoanzishwa mwaka 2013, umekuwa ukipanda mwaka hadi mwaka.
Akitoa mfano amesema, katika mtihani wa kuhitimu kidato cha sita mwaka 2024, jumla ya wahitimu 169 walifanya mtihani huo wavulana wakiwa 111 na wasichana 58 ambapo kati yao, watahiniwa 129 walipata daraja la I, 40 walipata daraja la II hakuna aliyepata daraja la III, daraja la IV wala daraja 0. ’Mafanikio haya ni makubwa na ni nia yetu kuyaenzi”, amesema. Sanjari na mafanikio hayo, shule ya sekondari ya Muyovosi iliyo umbali wa kilometa 34 kutoka Kasulu mjini, inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwepo ya ukosefu wa usafiri kwa ajili ya wanafunzi na walimu hasa inapotokea dharula.
Changamoto nyingine kwa mujibu wa mkuu wa shule hiyo ni upungufu wa walimu ikilinganishwa na tahasusi zilizopo, upungufu wa samani na uchakavu wa ofisi.
Shule ya sekondari ya Muyovosi inayotumia baadhi ya majengo yaliyokuwa makazi ya wakimbizi, inakabiliwa pia na uchakavu wa nyumba za walimu wanaoishi kwenye majengo hayo.
Akijibu risala katika mahafali hayo, mgeni rasmi ameahidi kuwa benki ya NMB itachangia viti na meza kwa ajili ya walimu ili kupunguza changamoto zinazoikabili shule hiyo.

Post a Comment