" WANANCHI 5000 KUNUFAIKA NA SKIMU YA UMWANGILIAJI

WANANCHI 5000 KUNUFAIKA NA SKIMU YA UMWANGILIAJI

 


Na Lucas Raphael,Tabora

 

Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imesaini mkataba wa Ujenzi wa skimu ya umwagiliaji uliyopo Kijiji Cha Idudumo kata ya Mwanzoli  wilaya ya Nzega mkoani Tabora  Mradi utakaongharimu kiasi cha  shilingi Billion 36.7

   Mradi huo utawanufaisha wananchi wapatao 5000 kutoka katika vijiji 5 vya  Idudumo,Mwanzori,Mwagedeli,Kitengwe na Iduguta katika kata za Mwanzori na Miguha na kuchochea uchumi wa wananchi wa kata hizo mbili.

 Akitoa taarifa ya Mradi huo baada ya utiaji saini na utekelezaji wa Mradi  huo Mhandisi wa Tume ya Umwagiliaji wa Mkoa wa Tabora Martin Mgangaluma  alisema kwamba wakulima watawezesha kulima katika misimu miwili.

 Alisema kwamba mradi huo  utainua Uchumi wa Mkulima Mmoja Mmoja na kuongeza usalama wa chakula katika Halmashauri ya Mji wa Nzega na Mkoa wa Tabora.

 Alisema kwamba Malengo  Mradi wa Ujenzi Skimu ya Idudumo ni kuongeza uwezo wa bwawa  kuhifadhi maji kutoka lita billioni 2.5 hadi kufikia Lita billioni  9 na kuongeza eneo la umwagiliji kutoka hekta 300 hadi  kufikia hekta 1,550.

 Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Uyui, Mohammed Mtulyakwaku akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora aliwataka wananchi kuutunza Mradi huo ili uweze kuwanufaisha na kizazi cha sasa na kijacho.

 Alisema wananchi hao wanapaswa kutumia mradi wa skimu kwa ajili ya kuinuka kimaisha na kuhakikisha waendelea na kilimo che tija .

 Mtulyakwaku  aliipongeza serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassani  kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kuendeleza mradi huo ambao utakuwa na tija kwa wananchi wa kata hiyo na vijiji jirani.

 Alisema kila mkulima wa vijiji hicho wanapaswa kuunga mkono juhudi za serikali ya wilaya na mkoa kwa ajili ya kuendelea mradi huo wa skimu.

 Aliwataka wananchi wote wa eneo la mradi kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi na kulinda miundombinu yote inayojengwa na Serikali kwa manufaa yao

 Nao wanufaika wa mradi huo wa Skimu aliishuru serikali ya awamu ya sita ambayo imetoa fedha nyingi kwa ajili ya kutekeleza mradi  mkubwa wa umwangiliaji .

 Mradi huo wa Ujenzi wa Skimu ya Idudumo unatekelezwa kwa awamu ya tatu katika Halmashauri ya Mji wa Nzega Mkoa wa Tabora.

 






Post a Comment

Previous Post Next Post