" WANAWAKE KILIMANJARO WAMPA KONGOLE MBUNGE ESTHER MALLEKO KWA MSAADA WA MASHINE ZA VIFARANGA

WANAWAKE KILIMANJARO WAMPA KONGOLE MBUNGE ESTHER MALLEKO KWA MSAADA WA MASHINE ZA VIFARANGA

Wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro wamempongeza Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Esther Malleko, kwa kutimiza ahadi yake ya kuwapatia mashine 169 za kutotolesha vifaranga vya kuku (incubators) kwa kata zote 169 za mkoa huo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mashine hizo, Mhe. Esther Malleko amesema lengo ni kuinua uchumi wa wanawake kupitia miradi ya uzalishaji wa vifaranga, kukuza lishe kwa jamii na kuimarisha mshikamano ndani ya chama na nje ya chama.

“Nimeleta IncubaTor kwa wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa kata zote 169, hizi nimezileta kimkakati. Siasa ni uchumi,”

“Nataka kuku hawa walete lishe kwenye jamii yetu kwa sababu mayai ni afya. Watoto wetu, wazee wetu, wamama wajawazito wote watapata mayai. Pia watakavyototolesha vifaranga, watawauza na kupata kipato mwanamke mmoja mmoja na vikundi vyote ambavyo nimeviunda kwenye kata.” amesema Malleko

Amesema mashine hizo zenye thamani ya Shilingi milioni 84.5 ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa wakati akiomba ridhaa ya kuwatumikia wanawake wa Kilimanjaro bungeni.

Mradi huo unatarajiwa kuwanufaisha wanawake katika kata zote za wilaya saba za Mkoa wa Kilimanjaro, ambazo ni: Moshi Manispaa, Moshi Vijijini, Hai, Siha, Rombo, Mwanga na Same

Katika kila wilaya, kata zote zimepangiwa mashine moja moja, kwa lengo la kuhakikisha kila eneo linapata fursa sawa ya kushiriki kwenye uchumi wa kisasa kupitia ufugaji wa kuku wa kisasa.

Baadhi ya wanawake waliofaidika na mradi huo wamesema kuwa mashine hizo zitawasaidia kujiondoa kwenye utegemezi wa mikopo yenye riba kubwa maarufu kama kausha damu, ambayo imekuwa ikiwatesa wanawake wengi wa mkoa huo na hata kusababisha kuvurugika kwa ndoa zao kutokana na presha ya marejesho.

"Wabunge wengine wa viti maalum waige mfano wa Mhe. Esther Malleko," wameeleza baadhi ya wanawake, wakisisitiza kuwa maendeleo ya wanawake hayapaswi kutegemea mikopo kandamizi bali misaada na miradi ya kuwawezesha kama huu.

Wanawake mbalimbali kutoka wilaya za mkoa huo, wakiwemo wa Wilaya ya Siha, wameeleza furaha yao na kumpongeza mbunge huyo kwa hatua hiyo muhimu ya kuwawezesha kiuchumi, wakisema mradi huo utaacha alama ya kudumu kwa wanawake wa Kilimanjaro.

Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Esther Malleko, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mashine za kutotolesha vifaranga vya kuku (incubators) kwa kata zote 169 za mkoa huo.

Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Esther Malleko, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mashine za kutotolesha vifaranga vya kuku (incubators) kwa kata zote 169 za mkoa huo.

 

Mmoja wa Wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro akimpongeza Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Esther Malleko, kwa kutoa mashine za kutotolesha vifaranga vya kuku (incubators) kwa kata zote 169 za mkoa huo.






 

Post a Comment

Previous Post Next Post