Wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro wamempongeza Mbunge
wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Esther Malleko, kwa
kutimiza ahadi yake ya kuwapatia mashine 169 za kutotolesha vifaranga vya kuku
(incubators) kwa kata zote 169 za mkoa huo.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi mashine
hizo, Mhe. Esther Malleko amesema lengo ni kuinua uchumi wa wanawake kupitia miradi ya
uzalishaji wa vifaranga, kukuza lishe kwa jamii na kuimarisha mshikamano ndani
ya chama na nje ya chama.
“Nimeleta
IncubaTor kwa wanawake wa Mkoa
wa Kilimanjaro kwa kata zote 169, hizi nimezileta kimkakati. Siasa ni uchumi,”
“Nataka
kuku hawa walete lishe kwenye jamii yetu kwa sababu mayai ni afya. Watoto wetu,
wazee wetu, wamama wajawazito wote watapata mayai. Pia watakavyototolesha
vifaranga, watawauza na kupata kipato mwanamke mmoja mmoja na vikundi vyote
ambavyo nimeviunda kwenye kata.” amesema Malleko
Amesema mashine hizo zenye thamani ya Shilingi
milioni 84.5 ni utekelezaji wa ahadi aliyotoa wakati akiomba ridhaa ya
kuwatumikia wanawake wa Kilimanjaro bungeni.
Mradi huo unatarajiwa kuwanufaisha wanawake katika
kata zote za wilaya saba za Mkoa wa Kilimanjaro, ambazo ni: Moshi Manispaa, Moshi
Vijijini, Hai, Siha, Rombo, Mwanga na Same
Katika kila wilaya, kata zote zimepangiwa mashine
moja moja, kwa lengo la kuhakikisha kila eneo linapata fursa sawa ya kushiriki
kwenye uchumi wa kisasa kupitia ufugaji wa kuku wa kisasa.
Baadhi ya wanawake waliofaidika na mradi huo
wamesema kuwa mashine hizo zitawasaidia kujiondoa kwenye utegemezi wa mikopo
yenye riba kubwa maarufu kama kausha damu, ambayo imekuwa ikiwatesa
wanawake wengi wa mkoa huo na hata kusababisha kuvurugika kwa ndoa zao kutokana
na presha ya marejesho.
"Wabunge wengine wa viti maalum waige mfano wa
Mhe. Esther Malleko," wameeleza baadhi ya wanawake, wakisisitiza kuwa
maendeleo ya wanawake hayapaswi kutegemea mikopo kandamizi bali misaada na
miradi ya kuwawezesha kama huu.
Wanawake mbalimbali kutoka wilaya za mkoa huo,
wakiwemo wa Wilaya ya Siha, wameeleza furaha yao na kumpongeza mbunge huyo kwa
hatua hiyo muhimu ya kuwawezesha kiuchumi, wakisema mradi huo utaacha alama ya
kudumu kwa wanawake wa Kilimanjaro.
Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Mhe. Esther Malleko, akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi mashine za
kutotolesha vifaranga vya kuku (incubators) kwa kata zote 169 za mkoa huo.

Mmoja wa Wanawake wa Mkoa wa Kilimanjaro akimpongeza
Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Esther Malleko, kwa kutoa mashine za kutotolesha
vifaranga vya kuku (incubators) kwa kata zote 169 za mkoa huo.

Post a Comment