Watu wasiojulikana wamevamia nyumbani kwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Mjini na kuteketeza gari huku, waliokuwa ndani wakinusurika kuungua moto unaodaiwa kuwashwa usiku wa kuamkia leo Aprili 22, 2025.

Tukio hilo linadaiwa kutokea nyumbani kwa kiongozi huyo huku watu takribani 11 waliokuwa ndani wakinusurika kuungua moto huo, ambao ulikuwa umeanza kuunguza vitu kwenye nyumba zilizopo eneo hilo.

Chanzo - Mwananchi