" WATANZANIA WAADHIMISHA KARUME DAY

WATANZANIA WAADHIMISHA KARUME DAY

Watanzania leo wanaadhimisha Karume Day, ikiwa ni kumbukizi ya kifo cha Hayati Abeid Amani Karume, Rais wa kwanza wa Zanzibar, aliyeuawa tarehe 7 Aprili 1972.

Abeid Karume alizaliwa tarehe 4 Agosti 1905 na anahesabiwa kama miongoni mwa viongozi waasisi wa Taifa, akiwa na mchango mkubwa katika kuleta Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 na baadaye kuunganisha visiwa hivyo na Tanganyika, hatua iliyozalisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Siku hii huadhimishwa kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na kitaifa ikiwa ni pamoja na mijadala ya kihistoria, ibada, na kuweka mashada ya maua kwenye makaburi ya viongozi wa kitaifa.

MISALABA MEDIA inawaalika Watanzania kuendeleza moyo wa uzalendo, mshikamano na amani kama alivyokuwa akihubiri mwasisi huyu wa taifa.


Post a Comment

Previous Post Next Post