
Dodoma
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ametoa rai kwa viongozi wa dini kuendelea kuliombea Taifa pamoja na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu..
Hayo yamesemwa leo (Aprili 19, 2025) Jijini Dodoma wakati wa Ibada takatifu ya kusimikwa kwa Askofu Mkuu Dkt. Evance Lucas Chande wa Karmeli Assemblies of God(KAG) ambapo Mh. Waziri Mkuu Majaliwa amewakilishwa na Waziri wa Madini Mh. Anthony Mavunde
“Serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mh. Rais Dkt . Samia Sukuhu Hassan imefanya kazi kubwa kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuishi katika misingi ya amani,umoja na mshikamano.
Nichukue fursa hii kutoa rai kwa viongozi wote wa dini zote kuliombea Taifa katika kipindi hiki tunapoelekea katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ili Tanzania iendelee kubaki moja, yenye amani na utulivu daima
“Baba Askofu Mkuu Dkt. Chande ni mmoja wa viongozi ambaye yupo karibu sana na jamii na amekuwa akijitoa sana kuwajali watu wengi wenye mahitaji, hivyo kupitia maombi ya kisima cha maji yaliyowasilishwa na kanisa tutahakikisha kanisa hili linapata kisima hicho mapema iwezekanavyo kwa kuwa tunajua pamoja na matumizi ya kanisa lakini maji hayo pia yatatumiwa na wananchi wa eneo la karibu na kanisa”Alisema Mavunde
Naye Askofu Mkuu wa KAG Dkt. Evance L. Chande ameishukuru Serikali kwa ushirikiano ambao amekuwa akiupata katika utoaji wa huduma ikiwa ni pamoja na uapatikanaji wa usajili wa huduma ya kanisa lake na kuwataka waumini wa kanisa hilo kumuweka katika maombi Mh. Rais Dkt. Samia na viongozi wote wa Tanzania.
Ibada ya kusimikwa Askofu Mkuu Dkt. Chande iliongozwa na Askofu Bernard Chinungo Mnasasi kutoka Nchini Kenya na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali mkoani Dodoma.







Post a Comment